DIWANI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIEZI SITA GEREZANI
Diwani
wa Kata ya Siuyu, Tarafa ya Mungaa (CHADEMA) jimbo la Singida
Mashariki, Jared Justin (34) ambaye ametumikia nafasi hiyo kwa kipindi
cha miezi minne na siku 22, amehukumiwa adhabu ya kutumikia jela miezi
sita baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuzuia wakala wa kukusanya
mapato ya halmashauri ya wilaya ya Ikungi.
Inadaiwa
kwamba jimbo hilo pekee mkoani Singida ambalo lipo mikononi mwa
upinzani (CHADEMA), lina sera ya kuzuia wananchi wake kuchangia
maendeleo yao kwa madai kuwa maendeleo ya wananchi ni jukumu la
serikali.
Mahakama
ya mwanzo ya Ikungi chini ya hakimu Simon Kiyinga, ilimuhukumu diwani
huyo kijana kwenda jela juzi mchana ambapo imedaiwa mahakamani hapo kuwa
mnamo Februari, 13 mwaka huu saa tatu asubuhi, katika mnada wa
njiapanda, mshitakiwa Jared alimzuia Afisa mwidhiniwa, Amina Abdallah wa
kampuni ya Abada Care Investment kufanya kazi ya kukusanya ushuru wa
halmashauri ya wilaya ya Ikungi.
Awali
ilidaiwa mahakamani hapo kuwa katika siku ya tukio, alitenda makosa
mawili ikiwa ni kumzuia Afisa Amina kufanya yake ya kukusanya mapato ya
halmashauri kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 12 para ya (e)
sheria ndogo ndogo ya halmashauri ya Ikungi.
Aidha,mshitakiwa
pia mshitakiwa alituhumiwa kutenda kosa la kushawishi wananchi waache
kuchangia mapato kwa halmashauri yao kinyume na sheria ndogo ndogo
kifungu cha 12 (1) (c).
Aidha
hakimu alitupilia mbali tuhuma ya kosa la pili kwa madai kukosekana kwa
ushahidi wa kutosha kumtia hatiani mshitakiwa diwani Jared.
Hakimu
Kayinga alisema kwa kosa la kwanza la kumuzuia afisa kukusanya mapato
yaliyobainishwa na halmashauri ya wilaya ya Ikungi, ushahidi wa upande
wa mlalamikaji umethibitisha bila kuacha shaka yoyote kuwa Jared kuwa
hatia kama ulivyoshtakiwa.
Kwa
hali hiyo, alisema mshitakiwa Jared atakwenda jela miezi sita ili iwe
fundisho kwake na kuogopesha madiwani wengine wanaotarajia kufanya kosa
la kuzuia kufanyika kazi halali.
Katika
kikao cha kwanza cha mkuu mpya wa Mkoa,Mathew Mtigumwe na viongozi
mbalimbali mkoani hapa,mkuu wa wilaya ya Ikungi Charles Gishuli,alisema
kuwa baada ya diwani huyo kumzuia wakala wa kukukusanya mapato alimwita
ofisini ili aende amwelemishe njia bora ya kutekeleza majukumu yake.
Alisema
diwani huyo alikataa akidai kwamba yeye hafanyi kazi chini ya DC na
ndipo serikali ya wilaya ilipofanya jitihada na kufanikiwa kuonana na
mkuu wa wilaya.
“Shida
yake huyu diwani wa CHADEMA, alikuwa anamlazimisha mkusanya mapato ampe
asilimia 20 za kijiji papo hapo kitendo ambacho ni kinyume na taratibu
na kanuni za halmashauri,” alisema Mkuu wa Wilaya.
Category:
0 comments