MAREKANI KUWATAHADHALISHA RAIA WAKE WALIOPO NCHI ZA ULAYA
Marekani imewaonya raia wake walio
Ulaya na wanaopanga kuzuru bara hilo kuhusu uwezekano wa kutokea kwa
mashambulio mengine ya kigaidi.
Wizaya ya mashauri ya kigeni ya Marekani imesema makundi ya kigaidi huenda yakatekeleza mashambulio karibuni.
“Makundi ya kigaidi yanaendelea kupanga mashambulio ya kuteketelezwa karibuni kote Ulaya, yakilenga hafla za michezo, maeneo ya kitalii, migahawa na uchukuzi,” taarifa ya wizara hiyo ilisema.
Raia wa Marekani wanaozuru Ulaya wametakiwa kuwa macho zaidi maeneo yenye watu wengi au wanapotumia mifumo ya uchukuzi wakati wa sikukuu ya Pasaka.
Miji mingi Marekani imeimarisha ulinzi katika viwanja vya ndege na vituo vya treni na mabasi.
Serikali hata hivyo imesema bado haina habari za uhakika kuhusu uwezekano wa kutokea kwa mashambulio Marekani.
Category:
0 comments