.

.

KUMEKUCHA LIBYA VIKOSI VYA LIBYA VYA TUPA MAKOMBORA KWENYE MAFICHO YA IS

ZePLAN | 21:58:00 |

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Libya amesema kuwa mateka wawili raia wa Italy waliotekwa nyara mnamo mwezi Julai huenda wameuawa nchini Libya kufuatia uvamizi wa vikosi vya Libya katika maficho yaliotumiwa na wapiganaji wa Islamic State.

Nyumba moja ya shambani kusini magharibi mwa mji wa Sabratha ilivamiwa kufuatia taarifa iliotolewa na wapiganaji wa Islamic State waliokamatwa wiki iliopita.

Meya wa Sabratha amesema  kwamba anaamini kwamba 2 kati ya 12 waliouawa katika shambulio hilo walikuwa wajenzi hao ambao ni raia wa Itali.
 
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Itali amesema kuwa bado anajaribu kuhakiki ripoti mbali na kuchunguza picha za waliouawa.

Raia 4 wa Itali kutoka kwa kampuni inayotoa huduma za mafuta na gesi Bonatti walitekwa nyara na watu wasiojulikana mnamo mwezi Julai,karibu na mpaka wa Libya na Tunisia.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!