KUNDI LA P-SQUARE MATATANI
Paul ameamua kujishusha na kumuomba msamaha kaka yake Peter Okoye.
Pacha huyo wa kundi la P-Square lililovunjika ameandika maelezo marefu kwenye Instagram kuelezea hali halisi ilivyo:Mnachotaka ni P-Square, ninachotaka ni familia, upendo na kujali. Mitandao ya kijamii ni mzizi mpya wa maovu. Kuna familia kabla ya Psquare na siku zote kutakuwepo familia baada PSquare. Jude alikuwa chambo na mhanga tu. Mtu ambaye amekuwa akituweka pamoja kwa miaka yote hii. Ukweli ni kwamba Peter na Paul wana matatizo.
Kwa mara ya kwanza nimeamua kufanya kitu nje ya Psquare, na huo ndio mfano hapa. Nimekuwa nikimuunga mkono kaka yangu kwa asilimia 100 kuanzia kwenye endorsement zake peke yake hadi kwenye Dance with Peter ambazo zingine bado zipo kwenye Instagram yangu.
Na sasa nina maswali matatu:
1.Kwanini haya mambo yanatokea muda mfupi baada ya kutoa single ya Muno chini ya Rudeboy Records?
2. Ni vipi baada ya Jude kuacha kuisimamia Psquare kwa zaidi ya mwezi sasa, matatizo bado yanaendelea?
3. Kwanini (Peter) ana haraka hivyo ya kuwa msanii anayejitegemea?
Inahuzunisha sana, na inavunja moyo sana, natamani mambo haya yasingefahamika hadharani. Na sasa mashabiki wetu wamegawanyika, tafadhali msiunge mkono ujinga wa teamPaul sihitaji hayo. Tafadhali mjizuie sababu ni uovu. Na kwa mapromota, kumuunga mkono Peter akitumbuiza nyimbo za PSquare peke yake jukwaani, mnatuua na kutuharibu sisi zaidi.
Mpendwa kaka yangU nakuomba, hata kama humtaki tena Jude na hauitaki psquare, milele utakuwa kaka yangu. Lakini natamani sisi watatu tungeendelea kuwa pamoja sababu ni kitu cha furaha. Watu wanatupenda sana si sababu tu ya muziki wetu mzuri, lakini kuwaona ndugu wakiwa pamoja, kuwa mfano mzuri kwa familia zingine na kwa watoto wetu. Tafadhali, jishushe, samehe na sahau, bado tunaweza kubadilisha hili jambo. Kama nilisema chochote au kufanya chochote nilichokuumiza, nisamehe. Na kwa mashabiki wetu wote wa ukweli, tafadhali tuombeeni. Mungu awabariki wote.
Category:
0 comments