WATUMIA JINA LA MKE WA RAIS KUFANYA UTAPELI
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imefafanua kwamba uchunguzi wao
umeonyesha kwamba Mke wa Rais, Mama Janet Magufuli hana akaunti ya
Facebook na tovuti inayohamasisha watu kuomba mikopo ya vikundi vya
Vicoba.
Mkurugenzi
Mkuu wa TCRA, Dr Ally Simba amesema Dar Es Salaam Jumamosi Machi 19
kwamba akaunti ya face book ambayo iliyodaiwa kuwa ni ya Mama Janet
ilianzishwa na matapeli wa mtandao.
Dr. Simba
alisema TCRA imeshafungia akaunti hiyo ya Facebook na tovuti
ya www.focusvikoba.wapka.mobi ambayo ilikuwa ina tarifa za kutaka
wananchi kutuma pesa za kiingilio kwa Vicoba ili wapate mikopo.
Dr. Simba
alisema ingawaje kumekuwepo na maendeleo na mabadiliko makubwa katika
sekta ya mawasiliano nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa
idadi ya watoa huduma za mawasiliano, idadi ya watumiaji na aina ya
huduma zinazotolewa kuna watumiaji wachache wanaotumia huduma hivyo
kutenda uhalifu kupitia simu za mkononi na kwenye intaneti kwa kuanzisha
tovuti za kihalifu na kupitia mitandao ya kijamii kama vile facebook.
Alisema
hivi karibuni kumekuwa na matukio ya wahalifu hawa wa mtandao kuanzisha
tovuti na blogu na pia kurasa za facebook kwa kutumia majina ya viongozi
wakuu wa nchi, wabunge na watu wengine maarufu.
Wahalifu
hawa wanawadanganya wananchi kwamba kuna fursa za kupata mikopo au
misaada kupitia vikundi vya kusaidiana, maarufu kama VICCOBA na kuwataka
wananchi watume fedha za kujiunga na huduma hizo kwa njia za simu za
mkononi.
Alisema
pamoja na kuzifungia akaunti hizo za facebook na tovuti, Mamlaka
inashirikiana na Polisi kuchunguza matukio hayo na tayari hatua kubwa
imefikiwa katika kuwakamata na kuwafikisha wahusika mbele ya vyombo vya
sheria.
Mkurugenzi
Mkuu alisema kwamba kwa mujibu wa kifungu cha 15 (1) cha Sheria ya
Makosa ya Mtandao ya 2015, mtu yeyote haruhusiwi, kwa kutumia kompyuta,
kujifanya yeye ni mtu mwingine15.
Adhabu
kwa kutenda kosa hili imeainishwa kwenye kifungu cha 15 (2) ambacho
kinasema mtu akipatikana na hatia anaweza kutozwa faini ya isiyopungua
shilingi milioni TANO au mara tatu ya thamani ya kile ambacho amekipata
kupitia ulaghai huo, au kiasi ambacho ni kikubwa kati ya faini na mara
tatu ya alichokipata. Vilevile anaweza kufungwa kifungo kisichopungua
miaka SABA au vyote.
Uchapishaji wa taarifa za uwongo ni kosa chini ya Kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya 2015.
Kwa
mujibu wa kifungu hicho, mtu yeyote ambaye anachapisha taarifa kwa
kutumia mfumo wa kompyuta akijua kwamba taarifa alizochapisha sio za
kweli, ni za udanganyifu na sio sahihi na kwa lengo ka kukashifu,
kutishia, kutukana,kudanganya na kuptosha umma anatenda kosa ambalo
adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi milioni TANO au kifungo miaka
mitatu au vyote.
Dr. Simba
aliwaomba wananchi kwa ujumla na hasa watumiaji wa huduma za
mawasiliano kuzingatia sheria wanapotumia huduma za mawasiliano.
Aidha
aliwataka Watanzania kuwa macho dhidi ya utapeli kupitia mitandao ya
kijamii, tovuti na blogu ambazo zinawataka kutuma fedha au kuchangia
kitu chochote ili wapewe mikopo au misaada. Wananchi wakiona matangazo
ambayo wanayatia shaka, wawasiliane na Mamlaka ya Mawasiliano kwa
taarifa zaidi.
Kuhusu
maendeleo ya sekta, alisema hadi Desemba 2015, idadi ya laini za simu za
mkononi ilikuwa 39,808,419 ukilinganisha na 2,963,737 mwaka 2005.
Watumiaji wa intaneti walifikia 17,263,523 Desemba 2015 ukilinganisha na
1,013,104 mwaka 2005.
Category:
0 comments