.

.

MABONDIA MADA MAUGO NA ABDALLAH PAZI KUKUTANA PASAKA HII UWANJA WANDANI TAIFA

ZePLAN | 01:01:00 | 0 comments

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ ambaye ni mratibu wa mpambano wa mabondia Mada Maugo kushoto na Abdallah Pazi akiwainuwa mikono juu kwa ajili ya kutambulisha mpambano wao wa ubingwa wa U.B.O Afrika utakaopigwa siku ya sikukuu ya pasaka katika uwanja wa ndani wa Taifa march 27

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ ambaye ni mratibu wa mpambano wa mabondia Mada Maugo kushoto na Abdallah Pazi akiwainuwa mikono juu kwa ajili ya kutambulisha mpambano wao wa ubingwa wa U.B.O Afrika utakaopigwa siku ya sikukuu ya pasaka katika uwanja wa ndani wa Taifa march 27.


MABONDIA Mada Maugo na Abdallah Pazi ‘Mfalme wa waalamu’ wamendelea kutambiana  kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya March 27 sikukuu ya Pasaka katika uwanja wa ndani wa Taifa akizungumza wakati wa kutambulisha mpambano huo.

Bondia Mada Maugo amesema kuwa Pazi ni mtoto mdogo sana katika ulimwengu wa masumbwi nchini hivyo inambidi afanye mazoezi ya kutosha ili avuke japo raundi ya nne mana sitakuwa na msalia mtume wakati wa kupambana pia naomba mashabiki zangu wafike mapema kwa ajili yakuona ninavyomsambalatisha Pazi mapema mana nimewapa bonanzi ya raundi nne mashabiki zangu akijibu mapigo hayo bondia Pazi amesema yeye kwa sasa ndio anatamba nchini hivyo yeye ni mfalme na akuna wa kuusambalatisha ufalme wake kwani kilicho mkuta bondia aliempiga China kwa K.o ya raundi ya tatu ndicho kitakacho mkuta yeye kwasababu amesha kuwa mzee sasa ni wakati wa damu changa pekee nae mratibu wa mpambano huo Rajabu Mhamila ‘Super D’ amesema mbali ya mpambano huo unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki lukuki kutakuwa na mipambano ya kukata na shoka ambapo bondia Nassibu Ramadhani atakumbana na Fansic Miyeyusho na bingwa wa mikanda miwili ya Afrika U.B.O na WPBF, Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ atkumbana na Deo Samweli na Pius Kazaula atakumbana na Seba Temba mpambano mwingine utawakutanisha Cosmas Cheka na Mohamed Matumla.

Katika mpambano uho kutakuwa na uhuzwaji wa vifaa vya mchezo wa ngumi pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa ajili ya kutambua sheria mbalimbali za mchezo zitakazokuwa zikitolewa bule kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa galama nafuu

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments