.

.

MH WILLIAM LUKUVI WAZIRI WA ARDHI AMEPOKEA MISSADA YA WAHANGA WA MAFURIKO MKOANI IRINGA

ZePLAN | 00:04:00 | 0 comments

vi2

Mhe. William Lukuvi akipokea msaada wa Wahanga wa mafuriko Isimani Iringa kutoka kwa Bibi Sawidath Mohamed Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) tawi la Dar es salaam akiwa na Bibi Rose Majuva Kamishna wa Makao Makuu  ya Taasisi hiyo (wa pili kulia) na Grace Shaba Naibu Katibu Mkuu TGGA.
vi3

Bibi Sawidath Mohamed Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) tawi la Dar es salaam akimkabidhi Mhe. William Lukuvi msaada wa Wahanga wa mafuriko Isimani Iringa.

vi1

Baadhi ya vitu alivyopokea Mhe. Lukuvi kwa ajili ya wahanga hao vikiwa katika gari ambavyo ni  Chakula, Nguo , viatu na Madaftari.

vi4 

Mhe. William Lukuvi akiwa na viongozi wa Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) ofisini kwake.Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi apokea Msaada kwa Wahanga wa mafuriko Iringa. Msaada huo ni kutoka Taasisi ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA) ambayo imemkabidhi Mhe. Lukuvi Unga kilo 155, Nguo na viatu balo 2, Sukari kilo 25 na Madftari Boksi 2 kwa ajili ya wahanga wa mafuriko jimboni kwake Isimaani.

Taasisi ya TGGA ni shirika lisilo la Kiserikali na ni chama cha kujitolea kinachojishughulisha na kuwaendeleza Wanawake pamoja na Watoto wa kike katika maswala ya kijamii na kiuchumi kwa kuwapa elimu na mafunzo.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments