MWANAJESHI WA AFRIKA KUSINI AUWAWA NCHINI SUDAN KATIKA SHAMBULIO LA KUSHTUKIZWA
Mwanajeshi kutoka Afrika kusini ameuawa nchini Sudan na mwingine kujeruhiwa baada ya kuviziwa katika jimbo la Darfur lililo magharibi mwa Sudan.
Jeshi la Afrika Kusini linasema kuwa wanajeshi hao walikuwa ni sehemu nya kikosi cha kulinda amani cha umoja wa mataifa, kilichokuwa kikisindikiza msafara wa shirika la mpango wa chakula duniani.Mwezi uliopita Afrika kusini ilisema kuwa ina mipango ya kuondoa wanajeshi wake kutoka Sudan, baada ya huduma ya miaka minane kwenye kikosi cha umoja wa mataifa.
Category:
0 comments