RISITI ZA IS ZANASWA NCHINI UJERUMANI
Maafisa wa polisi wa Ujerumani wanachunguza nakala zinazodaiwa kutambulisha idadi kubwa ya wapiganaji wa Islamic State.
Faili hizo zilizopatikana na vyombo vya habari vya Ujerumani na Uingereza zinasemekana kuwa za maswali yanayowabaini maelfu ya mashabiki wa kundi la Islamic State kutoka mataifa 50.Nakala hizo zinaorodhesha majina,maeneo wanaoyoishi na nambari za simu za wapiganajai hao.
Maafisa wa Ujerumani wanasema kuwa wanaamini kwamba huenda faili hizo ni za kweli.
Taarifa ya wizara imesema kuwa stakhabadhi hizo zinatoa fursa kuwatambua raia wa Urejumani wanaoshiriki katika maswala ya kigaidi ya kundi la IS.
Category:
0 comments