PAUL SCHOLES MAN UNITED HAIFAI
Manchester United ilikuwa haifai na
haikuwa na mpangilio wowote ilipofungwa 2-0 na Liverpool kulingana na
Paul Scholes ambaye alikuwa kiungo wa kati wa timu hiyo Paul Scholes.
Scholes ambaye aliichezea Manchester United mara 718 aliambia BT Sport kwamba kilabu hiyo ya Old Trafford huwa na viwango fulani lakini kufikia sasa imefeli kuafikia viwango hivyo.
Aliongezea:Liverpool ilikuwa na mpango wa kucheza,Lakini United hawakuwa na mpango wowote.
Awamu ya pili ya mechi ya marudiano itachezwa katika uwanja wa Old Trafford Alhamisi ijayo.
''Manchester United inafaa kuwania ligi ya Uingereza na kombe la vilabu bingwa'',alisema Scholes.
Wametumia pauni milioni 300 na bado wako katika nafasi ya sita katika jedwali la ligi.
Wameshushwa hadi katika ligi ya Europa baada ya kushindwa katika kombe la vilabu bingwa.
Wanafaa kushindana na Barcelona,Real Madrid na Bayern.
Category:
0 comments