LIVERPOOL YAILAZA MAN UNITED MBILI KWA NUNGE (2-0)
Liverpool ilichukua udhibiti wa
kombe la bara Europa baada ya kuifunga timu ya Manchester United
iliokuwa ''haijiwezi'' katika uwanja wa Anfield.
Danniel Sturidge aliifungia Liverpool bao la kwanza kunako dakika ya 20 baada ya mchezaji wa Manchester United Memphis Depay kumuangusha Nathaniel Clyne kabla ya Roberto Firmino kuongeza bao la pili akiwa karibu na goli ikiwa imesalia dakika 17 pekee.
United hawakupata hata nafasi moja na ni mchezo mzuri wa kipa De gea uliozuia mashambulizi ya Liverpool.
Category:
0 comments