PICHA MBALIMBALI ZA MSANII LADY JAY DEE KWENYE SHEREHE YA UZINDUZI WA NYIMBO YAKE NDI NDI NDI
Usiku
wa Jumamosi katika Ukumbi wa Sky Night Life uliopo Masaki, Dar es
Salaam kulifanyika halfa ya kusikiliza wimbo mpya wa mwanamuziki Lady
Jay Dee ‘Listening Party’ uliyopewa jina la Ndi Ndi Ndi.
Unaweza kutizama picha jinsi Listening Party hiyo ulivyokuwa ambapo nyimbo hiyo inataraji kuwepo hewani kupitia mtandao wa Mkito.com kuanzia Jumapili ya Machi, 20.
Lady Jay Dee katika pozi baada ya kuwasili ukumbini katika ‘Listening Party’ ya wimbo wake mpya.
Baadhi ya wageni waliohuduria halfa hiyo iliyofanyika Sky Night Life iliyopo Masaki, Dar es Salaam
Meneja wa Lady Jay Dee, Seven Mosha akitoa neno la ufunguzi katika ‘Listening Party’ ya wimbo mpya wa Komando Jide – Ndi Ndi Ndi
Lady
Jay Dee akisaini mkataba na Mkito kwa ajili ya kuwapa haki za kuweka
nyimbo yake mpya katika mtandao huo. Kushoto ni Meneja Biashara wa
Mkito, Aishi Mengi.
Meneja
Biashara wa mtandao wa Mkito, Aishi Mengi akisaini mkataba wa kuwapa
haki ya kuweka nyimbo mpya ya Lady Jay Dee katika mtandao wa Mkito.com
Meneja Biashara wa mtandao wa Mkito, Aishi Mengi na Lady Jay wakikabidhiana mikataba baada ya kuwekeana saini.
Meneja Biashara wa mtandao wa Mkito, Aishi Mengi akitoa neno la shukrani kwa Lady Jay Dee
Lady Jay Dee akiwashukuru Mkito. Kushoto ni Meneja Biashara wa mtandao wa Mkito, Aishi Mengi
Lady
Jay Dee akizungumza kuhusu watu ambao wamekuwa wakishirikiana nae
katika kipindi cha furaha na huzuni kabla ya kuanza kutoa tuzo.
Tuzo ambazo Lady Jay Dee ametoa kwa watu wake wa karibu.
Lady Jay Dee akimtaja mtu wa kwanza kuchukua tuzo ambaye alikuwa ni rafiki yake, Abdallah.
Lady Jay Dee akimkabidhi tuzo ya Abdallah kwa kumpa ‘support’ katika muziki wake.
Lady Jay Dee akimkabidhi tuzo mdau wake wa karibu, Edward.
Komando Jide akimkabidhi tuzo msanii mwenzake Rama Dee
Lady Jay Dee akimkabidhi tuzo Monica Joseph akimwelezea kama mtu ambaye amekuwa akimsaidia pindi anapoyumba kifedha.
Lady Jay Dee akimkabidhi tuzo ya heshima rafiki yake, Mbunge wa viti maalum CCM Arusha, Mh Catherine Magige.
Lady Jay Dee akimkabidhi tuzo Lucy Mosha kwa kuwa shabiki ambaye anam’support’.
Jide akimkabidhi tuzo, Dj Choka.
Lady Jay Dee akimkabidhi tuzo rafiki yake Dori kwa kuwa mtu ambaye ana msaada katika maisha yake.
Mwakilishi wa CRDB Bank akipokea tuzo kutoka kwa Lady Jay Dee kwa ‘support’ wanayompa.
Lady Jay Dee akimkabidhi tuzo Khadija Mwanamboka.
Komando Jide akimkabidhi tuzo rafiki yake, Anita.
Jessica Malembeka akipokea tuzo kutoka kwa Lady Jay Dee katika halfa ya uzinduzi wa nyimbo ya Jide – Ndi Ndi Ndi
Lady Jay Dee akipokea zawadi kutoka kwa rafiki yake Ester Fayard.
Komando Jide akionyesha zawadi ambayo amepokea kutoka kwa Ester Fayard.
Komando Jide akiwa katika pozi la furaha na marafiki zake waliojumuika pamoja naye katika ‘Listening Party’ ya nyimbo yake mpya, Ndi Ndi Ndi.
Lady Jay Dee akizungumza na marafiki zake wa karibu. Kulia ni msanii mwenzake, Wakazi.
Lady Jay Dee akimwambia jambo Wakazi.
Category:
SAFI
ReplyDelete