Truong Tan Sang
Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang akizungumza na viongozi mbalimbali toka Tanzania na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Truong Tan Sang
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akigonga glass na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang ikiwa ni ishara ya ushirikiano kati ya Tanzania na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Janeth Magufuli

 Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang akigonga glass na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.\

Truong Tan Sang

Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang (Kulia) akiwa amenyanyua glass juu pamoja na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa,Majaliwa ikiwa ni ishara ya kutakia heri kati ya Tanzania na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

John Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang wakitoa heshima kwa nyimbo za mataifa hayo mawili.

Aldof Davis Mwamunyange

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Generali Aldof Davis Mwamunyange (Wa pili kulia) akifatilia hotuba za Rais wa Tanzania na Vietnam katika halfa ya kumkaribisha iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspecta Generali Ernest Mangu, wa pili kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Magereza Kamishna Jenerali Casmir Minja, katikati ni Mkuu wa Usalama Rashid Othman na kushoto ni Kamanda wa Kanda maaalum Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro.

John Kijazi

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (katikati) akifatilia halfa ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti Mhe. Truong Tan Sang iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam kushoto ni Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kushoto ni Mnadhimu Mkuu mstaafu wa Jeshi la wananchi la Tanzania Luteni Generali Abdulrahman Shimbo.