.

.

TRUMP ABWAGWA NA TED CRUZ HUKU BERNIE SENDERS AKISHINDA NA KUMWAGA BI HILLARY CLINTON KWA KISHINDO

ZePLAN | 23:20:00 | 0 comments

Sanders 

Bernie Sanders amemshinda Hillary Clinton katika mchujo wa chama cha Democratic uliofanyika katika jimbo la Maine.

Baada ya 91% ya kura kuhesabiwa, seneta huyo wa Vermont ana 64%, huku Clinton akiwa na 36%.
Katika chama cha Republican, Marco Rubio ameshinda kwa urahisi mchujo katika eneo la Puerto Rico, na kumbwaga bilionea Donald Trump.

Bi Clinton na Bw Trump hata hivyo bado wanasalia kuongoza kwa jumla katika kinyang’anyiro cha kuteua mgombea urais wavyama vya Democratic na Republican mtawalia.

Jumapili usiku Bi Clinton na Bw Sanders walikabiliana vikali kuhusu masuala kadha, ikiwemo sera ya kiuchumi, katika mdahalo wa runingani ulioandaliwa na runinga ya CNN katika mji wa Flint, Michigan.
Kwenye mchujo uliofanyika Jumamosi, Bw Sanders alishinda majimbo mawili - Kansas na Nebraska – lakini Bi Clinton akasalia bado kuwa mbele chama cha Democratic baada ya ushindi mkubwa Louisiana.

Ingawa ushindi wa Bw Rubio katika eneo la Puerto Rico, linalomilikiwa na Marekani, utaimarisha matumaini Bw Rubio, ambaye ni gavana wa Florida, umemzolea wajumbe 23 pekee.

Cruz
Ted Cruz na Donald Trump bado wanaongoza kinyang'anyiro cha Republican
 
Wagombea wa Republican wanahitaji kupata wajumbe 1,237 ili kutwaa tiketi ya kupeperusha bendera ya chama hicho uchaguzi wa urais mwezi Novemba.
Bw Rubio bado yuko nyuma ya Donald Trump anayeongoza na seneta wa Texas Ted Cruz aliye wa pili.
Kwa sasa katika ratiba ya mchujo macho yanaelekezwa kwa:
  • 8 Machi: Michigan na Mississippi mchujo wa Democratic na Republican; na mchujo wa chama cha Republican Hawaii na Idaho.
  • 15 Machi: Mchujo wa Democratic na Republican katika majimbo ya Florida, Illinois, Missouri, North Carolina na Ohio.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments