.

.

WANNE WAKAMATWA NA POLISI KWA KUKODISHA RANCHI YA MISENYI KWA WANANCHI

ZePLAN | 01:56:00 | 0 comments

Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Festo Kiswaga

Akitoa amri ya kukamatwa kwa Watumishi hao Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Festo Kiswaga, aliamuru maafisa hao wanne ambao ni Afisa wa Mifugo wa wilaya ya Misenyi, Steven Makula, Afisa Mifugo, Kata ya Kakuru, Eric Kagoro, Meneja wa Ranchi Martin Ladslaus, pamoja na Msaidizi wake kedmund Aloyce.

Akiwasomea tuhuma zinazowakabili watumishi hao ni pamoja na kusingizia kuwa wametumwa na uongozi wa juu kukodisha ranchi hiyo lakini pia ikiwa ni pamoja na kuchukua fedha ambazo walidai ni tozo la kuingiza mifugo katika ranchi hiyo.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amependekeza vyombo vya ulizn ina usalama wilayani humo ikiwemo Takukuru kufanya uchunguzi wa kina juu ya Watumishi hao na nedapo watabaika kuwa na tuhuma za kujibu wafunguliwe mashataka mara moja.

Hivi karibuni Waziri Mkuu alifuta vitalu saba vilivypo katika ranchi ya Misenyi, ikiwa ni pamoja na kitalu namba moja,Kitalu namba tano, kitalu namba saba , kitalu namba tisa, kitalu namba kumi,kitalu namba 11, pamoja na kitalu namba 12 baada ya kubainika na kujihusisha na kuingiza Ng'ombe kutoka nchi Jirani.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments