MSHUKIWA MKUU WA TUKIO LA PARIS NCHINI UFARANSA ATIWA NGUVUNI
Maafisa wa polisi nchini Ubelgiji wakimkamata mshukiwa
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameonya kuwa mitandao ya kigaidi barani Ulaya inaendelea kuimarika licha ya kukamatwa kwa mmoja wa washukiwa wa mashambulizi ya mwezi Novemba mjini Paris.
Salah Abdeslam alikamatwa wakati wa uvamizi uliofanywa na kikosi cha kupambana na ugaidi nchini Ubelgiji katika wilaya ya Molenbeek mjini Brussels baada ya kupigwa risasi kwenye mguu.
Eneo lililovamiwa na maafis wa polisi
Mtu mwingine ambaye pia anashukiwa kuhusika kwenye mashambulizi hayo ya mwezi Novemba alijeruhiwa na kukamatwa na kwa ujumla watu watano walikamatwa.
Maafisa wa polisi
Bwana Hollande alisema kuwa vita havitakwisha hadi kila mmoja aliyehusika kwenye shambulizi la Paris akamatwe.
Watu 130 waliuawa wakati wa shambulizi hilo.
Category:
0 comments