Yanga vs Al Ahly 
Baada ya sare ya goli 1 – 1 kati ya Yanga na APR katika Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam, mabingwa hao wa Tanzania wamefanikiwa kufuzu hatua inayofuata ya Kombe la Mabingwa Afrika kwa kuwa na ushindi wa jumla ya magoli 3 – 2.

Yanga inataraji kukutana na Al Alhy ya Misri ambayo nayo iliibuka na ushindi wa goli 2 – 0 kwa bila dhidi ya Libolo ya Angola.

Aidha mchezo wa kwanza  wa Yanga na Alhy unataraji kuchezwa Tanzania Aprili, 9 na marudio yanataraji kuwa Aprili, 19 nchini Misri.