AL- SHABAAB WAENDELEA KUSHAMBULIWA ZAIDI NA JESHI LA MAREKANI
Jeshi la Marekani limesema kwamba lilitekeleza mashambulio ya anga nchini Somalia na kuwaua wapiganaji 12 wa kundi la Al Shabaab. Idara ya ulinzi imesema wapiganaji hao walitishia usalama wa maafisa wa Marekani ambao wanasaidia wanajeshi wa serikali ya Somalia.
Wakaazi wa maeneo kulikofanyika mashambulio hayo wamesema baadhi ya waliouawa walikua ni raia. Haya ndiyo mashambulizi ya hivi karibuni ya Marekani nchini Somalia dhidi ya kundi la Al Shabaab ambalo linashirikiana na mtandao wa Al Qaeda.
Wiki jana idara ya ulinzi ya Marekani ilisema kiongozi mmoja wa Al Shabaab Hassan Ai Dhoore alikua ameuawa kwenye shambulio la ndege isiyo na rubani. Wapiganaji hao wamekua wakitekeleza mashambulizi makali dhidi ya maafisa wa serikali ya Somalia, wanajeshi wa kigeni sawa na kulenga hoteli na migahawa katika mji mkuu Mogadishu.
Category:
0 comments