DRC YASHAMBULIWA NA HOMA YA MANJANO 21 WAPOTEZA MAISHA
Mulipuko wa homa ya manjano umewaua watu 21 katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani{WHO}, homa hii imetoka katika nchi jirani ya Angola.
WHO imeongeza kwamba maafisa wa DRC wameweka vituo vya dharura kushughilikia mulipuko huo.Aidha raia wanaosafiri nchini Angola watapewa chanjo dhidi ya ugonjwa huo. Homa hii husababisha kuvuja damu na figo kushindwa kufanya kazi.
Inaambukizwa na aina ya mbu {Aedes aegypti}. Maeneo yaliyo kwenye hatari ya Homa ya manjano ni pamoja na Bara Afrika na Amerika Kusini.
Category:
0 comments