CHINA YAPIGA MARUFUKU NDOA YA JINSIA MOJA
Jaji nchini China ametoa amri ya kutupilia mbali ombi la mwanamme ambaye alitaka utawala kumtambua yeye na mpenzi wake wa kiume kuwa wanandoa halali.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 26, Sun Wenlin alishtaki baraza la mji wa Changsha baada ya maafisa kupuzilia mbali ombi lake la usajili kile ambacho wawili hao walikiita ndoa.
Waliowaunga mkono walikusanyika katika mahakama hiyo. Wenlin amesema kuwa atakata rufaa.
Wapenzi wa jinsia moja nchini China hukusanyika katika sherehe za umma na kutangaza muungano wao, ama huoana katika sehemu za nchi za nje lakini ndoa hizo hazitambuliwi kisheria.
Category:
0 comments