HATRICK YA ANDY CAROLL YAVUNJA MATUMAINI YA UBINGWA KWA ARSENAL
Andy Caroll alifunga mabao matatu na
kuiwezesha West Ham kuizuia Arsenal na hivyobasi kuvunja matumaini ya
timu hiyo kushinda taji la ligi ya Uingereza.
Mesut Ozil na Alexis Sanchez waliiweka Arsenal kifua mbele kufuatia pasi nzuri za Iwobi ,lakini Caroll alifunga mabao mawili ya ghafla ndani ya sekunde 160 ili kusawazisha.
Kichwa kizuri katika kipindi cha pili kilimpatia Andy Caroll bao lake la tatu ,kabla ya beki wa Arsenal Laurent Koscielny kusawazisha.
Hatahivyo West Ham iliongeza rekodi yake ya kutofungwa katika ligi ya Uingereza na kufikia mechi 14 wakiwa nyumbani ,lakini kikosi hicho cha kocha Slaven Bilic kinasalia nafasi ya sita katika jedwali la ligi ya Uingereza.
Category:
0 comments