Mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza kati ya Swansea iliyokuwa mwenyeji wa Chelsea katika uwanja wake wa nyumbani wa Liberty umemalizika kwa Swansea kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila.

Goli pekee la Swansea limefungwa na Gylfi Sigurdsson katika dakika ya 25 baada ya kuunganisha mpira uliotolewa langoni kwa goli la  Chelsea na beki Miazga, goli lililodumu hadi dakika ya mwisho ya mchezo huo.

Baada ya matokeo hayo, Swansea imekuwa timu ya kwanza kumfunga kocha wa Chelsea, Guus Hiddink baada ya kuiongoza timu hiyo kwa michezo 15 ya Ligi Kuu ya Uingereza bila kupoteza mchezo wowote.