.

.

IRAN INAUZA MAPIPA MILIONI MBILI KILA SIKU

ZePLAN | 18:30:00 | 0 comments

 


Uuzaji wa mafuta ya Iran umefikia kiwango kikubwa zaidi cha mapipa milioni mbili kwa siku kwa mara ya kwanza tangu kuondolewa vikwazo vya kiuchumi mapema mwezi Januari.

Wachanganuzi wa masuala ya kiuchumi wanasema Iran, itaendelea kuongeza kiwango cha uzalishaji na uuzaji wa mafuta yake nchi za nje hadi itakaporejelea kiwango chake cha mapipa milioni 2 na laki tano ilichokuwa ikiuza ng'ambo kabla ya kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.
 
Iran, itaendelea kuongeza kiwango cha uzalishaji na uuzaji wa mafuta yake nchi za nje hadi itakaporejelea kiwango chake cha mapipa milioni 2 u nusu
Habari hiyo hata hivyo haisaidii mataifa wauzaji wa mafuta ambao kwa sasa wanateswa na bei iliyoporomoka ya mafuta katika soko la dunia.

Bei ya mafuta imekuwa ikiporomoka kwa takriban mwaka mmoja sasa kufuatia uzalishaji mkubwa uliofanya bidhaa hiyo kukosa soko.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments