Staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amezidi kuonyesha kuwa yeye ni bora katika soka baada ya kufunga goli katika mchezo wa leo dhidi ya Eibar ambalo limemuwezesha kujiwekea rekodi mpya katika klabu yake.

Baada ya kufunga goli hilo Ronaldo amefikisha magoli 30 kwa msimu wa 2015/2016 na kufikisha misimu sita mfululizo akifikisha idadi hiyo ya magoli.

Msimu wa 10/11 (41), 11/12 (46), 12/13 (34), 13/14 (31) and 14/15 (48).

Wachezaji wengine waliofunga magoli katika mchezo wa Eibar ni James Rodriguez dk. 5, Lucas Vazquez dk. 18, Cristiano Ronaldo dk. 19 na Jese Rodriguez katika dakika ya 39.