MKUU WA MKOA WA MBEYA APITISHA MSAKO WA PILI JUU YA WAFANYAKZI HEWA
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh AMOS MAKALA ametoa agizo la kuhakiki wafanyakazi hewa mkoani kwake ili aweze kujiridhisha juu ya uwepo wa wafanyakazi halali na kuwabaini wafanyakazi hewa mkoani humo.
Zoezi hili linaendeshwa na timu ya watu 16 ambao wanakazi yakupitia na kukagua wilaya zote ilikubaini kama kuna wafanyakazi hewa ambao walisalia baada ya msako wa kwanza kupita na kutokugundulika.
Mh Amos Makala ambae aliwahi kushika hatamu za uongozi sehemu mbali mbali ikiwemo ubunge katika wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro na kupanda ngazi mpaka kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro anaendelea kufanya vyema katika utendaji wake na kuonyesha dhamira za dhati kabisa za kuleta maendeleo mkoani humo.
Category:
0 comments