.

.

UFAFANUZI JUU YA MIL 50 ZA KILA KIJIJI WAWEKWA BAYANA

ZePLAN | 01:24:00 | 0 comments

Image result for KASIMU MAJALIWA DODOMA
Picha juu waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa


Dodoma. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imetenga Sh59 bilioni kwa ajili ya utekelezaji wa ugawaji wa Sh50 milioni kwa kila kijiji nchini zilizoahidiwa na Rais John Magufuli wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita.

Akijibu hoja za wabunge walizozitoa wakati wa mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu mwaka 2016/17, Majaliwa alisema mradi huo unalenga kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kutenga fedha hizo kwa kila kijiji kama Mfuko wa Uwezeshaji kwa ajili ya kukopesha vikundi vya wajasiriamali kupitia ushirika wa kuweka na kukopa.

Hata hivyo, wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha vifungu vya bajeti hiyo, Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT – Wazalendo), Zitto Kabwe alisema fedha hizo hazijatengwa katika Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu wala ile ya Ofisi ya Rais – Tamisemi iliyotarajiwa kuwasilishwa jana jioni.

Kutokana na suala hilo kuibua mvutano mkali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson walikiri jambo hilo na kumtaka Zitto kusubiri bajeti ya Tamisemi kwanza jambo ambalo lilipingwa na mbunge huyo kwa maelezo kuwa hata katika bajeti ya Tamisemi, fedha hizo hazijatengwa na kutaka kuelezwa zilipo. 

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments