.

.

KOREA KASKAZINI YAIPANDISHA PRESHA MAREKANI

ZePLAN | 05:08:00 | 0 comments

Korea Kaskazini yadai uwezo wa kulipua Marekani                

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, amesema kuwa taifa lake linauwezo wa kushambulia maeneo ya Marekani, katika bahari ya Pacific.

Rais Kim Jong alisema hayo baada ya taifa lake kufanikiwa kutekeleza majaribio ya makombora yenye uwezo wa kusafiri mwendo wa kasi hadi masafa ya kadri.

                Rais Kim akishuhudia majaribio ya silaha                
Runinga ya taifa mjini Pyongyang, imetangaza kuwa bwana Kim Jong mwenyewe alisimamia na kushuhudia majaribio hayo ya silaha hatari ya masafa ya kadri.
Wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa wamekutana                
Wataalamu wa kijeshi wa Marekani na Korea Kusini wanasema kwamba kombora moja lilishindwa kulipuka ilihali la pili ilifaulu kwenda zaidi ya mamia ya kilomita.

Korea Kaskazini imesifia vikukubwa uwezo wake huo wa kuunda silaha za kitonoradi.
             
Wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa wamekutana na kuelezea kutamaushwa kwao na hatua hiyo ya Korea Kaskazini.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments