KOREA KASKAZINI YARUDIA KAMCHEZO KAKURUSHA MAKOMBORA
Korea Kusini
inasema kuwa majirani zao Korea Kaskazini kwa mara nyingine tena,
wameifanyia majaribio makombora yake mawili, hatua ya wazi ya kuonesha
kukiuka hatua Umoja wa mataifa kuiwekea taifa hilo vikwazo vya kiuchumi.
Taarifa zasema kombora la kwanza halikufanikiwa huku la pili likisafiri
umbali wa kilomita mia nne.
Msemaji wa Waziri wa Umoja wa taifa wa Korea Kusini Joeng Joon-hee amesema majaribio hayo ni kukiuka vikwazo.
"Ulipuaji
huo makombora kwa kutumia Teknolojia ya angani unakiuka maazimio ya
Umoja wa mataifa. NIa ni uchokozi dhidi yetu. Tunashauri ni vyema kwa
Korea Kaskazini kuzidisha nguvu katika kuimarisha amani katika eneo la
rasi ya Korea na kwa maisha ya watu wake ambayo Korea kaskazini imekuwa
ikisititiza kila wakati." Amesema
Naye waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amelaani hatua hiyo Korea ya Kaskazini.
"Leo
kumelipuliwa makombora kwa kutumia teknolojia ya angani iliyotumika
zamani huu ni ukiukwaji wa wazi wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja
wa mataifa. hatutarusu na tutaandaa azimio la kupinga hatua hiyo,"
amesema Waziri Mkuu huyo
Category:
0 comments