.

.

MBUNGE WA SINGIDA MASHARIKI ALALA RUMANDE BAADA YA KUKOSA DHAMANA

ZePLAN | 22:43:00 | 0 comments


Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amewekwa rumande kwa kukosa dhamana, mara baada ya mahojiano na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kwa masaa kadhaa kufuatia kauli yake aliyoitoa jana inayoelezwa kuwa haikuwa nzuri.

Kukosa dhamana hiyo kunafuatia kwa  Mbunge Lissu kuripoti  katika kituo cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa na Jeshi hilo kuhusu kauli yake aliyoitoa jana baada ya kutoka mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Mbunge huyo amehojiwa kwa saa tatu  kuhusiana na maneno mengine ambayo anayodaiwa kuyaandika kupitia mitandao ya kijamii kuwa ni ya uchochezi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam leo, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekili kuwa Lissu amewekwa rumande kwa kukosa dhamana na hataachiwa leo, hivyo atalala huko mpaka kesho.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments