.

.

KOREA KASKAZINI YARUSHA MAKOMBORA MATATU YA MASAFA MAREFU

ZePLAN | 01:51:00 | 0 comments

Makombora ambayo Korea Kaskazini ililipua hivi karibuniMakombora aina ya Scud 
 

Jeshi la Korea Kusini linasema Korea Kaskazini imerusha makombora matatu ya masafa marefu baharini saa chache baada ya Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye kukutana na Rais wa Uchina Xi Jinping pambizoni mwa mkutano mkuu wa nchi 20 zenye zilizostawi zaidi kiuchumi duniani.
Makombora hayo yalirushwa kutoka eneo la Hwangju.
Bi Park ametoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano zaidi na Uchina, ambayo ni mshirika wa Korea Kaskazini, kuhusu kile alichosema ni uchokozi wa mara kwa mara wa Pyongyang ambayo imekuwa ikifanya majaribio ya mabomu ya nyuklia na makombora.

Vyombo vya habari Uchina vimesema Xi amesisitiza pingamizi zake dhidi ya kujengwa kwa mfumo wa Marekani wa kujikinga dhidi ya makombora nchini Korea Kusini.
Amesema mpango huo huenda ukazidisha uhasama.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments