.

.

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAKANUSHA KUHUSU KUJIUZULU KWA MAKAMU WA RAIS

ZePLAN | 01:43:00 | 0 comments

 
Taarifa iliyotolewa na ofisi hiyo kwa vyombo vya habari imesema kwamba taarifa hizo kumuhusu Makamu wa Rais ni za uzushi na uongo na kwamba hazina ukweli wowote.


Taarifa hiyo imeendelea kufafanua kuwa habari hizo ni za uchochezi na kwamba zinalenga kuliweka taifa kwenye taharuki. 

 
Imesema kuwa Mhe. Makamu wa Rais yuko bega kwa bega na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba ya nchi ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Ofisi ya Makamu wa Rais imewataka wananchi na watanzania kwa ujumla kupuuza taarifa hiyo ambayo ofisi hiyo imeilezea kuwa inalenga kupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Viongozi hao.

Ofisi hiyo pia imewasihi Watanzania kufanya kazi kwa bidii na wajiepushe na vitendo vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu nchini.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments