ANAE JIITA NABII AWANYWESHA WATU KEMIKALI AFRIKA KUSINI
Mtu mmoja anayejiita nabii nchini Afrika Kusini amesababisha wafuasi
wake kunywa kemikali ya kusafisha injini, akidai kuwa ina uwezo wa
kuponya na ina ladha ya asali.
Theo Bongani Maseko wa kanisa la
Breath of Christ Ministries, anasema kuwa kemikali hiyo hushambulia
virusi kwenye mwili wa binadamu, na kutambua mashetani.
Mtu huyo
ni kati ya wanaume kadha ambao wamezua shutuma kwa kuwamwagia watu dawa
ya kuuaa wadudu na pia kuwashauria kula wanyama.
Bwana Maseko alinukuliwa akisema kuwa kemikali hiyo haina athari za kiafya.
"Ina ladha ya asali , nimekunywa mara mbili."
Aliongeza kuwa watu watatu wameponywa kwa kunywa kemikali hiyo.
Category:
0 comments