DONALD TRUMP ATOA AHADI YA KUSHIRIKIANA NA KUWAJALI RAIA WOTE NCHINI MAREKANI
Donald Trump ameahidi kuwaunganisha
Wamarekani alipokuwa anawahutubia wafuasi wake wakati wa tamasha la
mkesha wa kuapishwa kwake kuwa rais.
Akiongea katika vidato vya sanamu ya ukumbusho wa Lincoln mjini Washington DC, rais huyo mteule pia aliahidi kuleta mabadiliko.
Miongoni
mwa waliohudhuria hafla hiyo iliyodumu saa mbili ni mke na watoto wake,
mwigizaji Jon Voight na mwanamuziki aliyeimba wimbo wa Soul Man, Sam
Moore.
Bw Trump baadaye aliweka shada la maua katika makaburi ya taifa ya Arlington, Virginia.
Rais Mteule Donald Trump akiweka shada la maua |
Hafla
hiyo ya Make America Great Again! (Fanya Marekani kuwa kuu tena)
ilikuwa wazi kwa umma kuhudhuria na miongoni mwa waliotumbuiza ni nyota
wa muziki wa country Toby Keith na Lee Greenwood.
Tazama video wakati Donald Trump akihutubia kwenye makumbusho
Category:
0 comments