.

.

SENEGL YAINGIZA VIKOSI VYAKE NCHINI GAMBIA MAPEMA LEO

ZePLAN | 01:03:00 | 0 comments

Gambia

Senegalese special operations forces conduct a beach landing exercise
Picha ni Vikosi vya Senegal vikiweka mashua yao sawa nchini Gambia
Msemaji wa jeshi la Senegal Kanali Abdou Ndiaye amesema kwamba vikosi hivyo vimevuka mpaka na kupiga hatua kuelekea katika mji mkuu wa nchi hiyo,Banjul.Na kusema kwamba vikosi hivyo mpaka sasa havijakabiliana na ukinzani wa aina yoyote ingawa viliweka bayana kwamba vilikuwa vimejizatiti kwa mapigano ikibidi.

Army chief General Ousman Badjie
Picha ni Kanali Abdou Ndiaye


Mapema baraza la usalama la Umoja wa mataifa inasemekana kwa siri limekuwa likiunga mkono juhudi za vikosi vya ECOWAS, kuhakikisha kwamba rais Barrow anachukua madaraka kutoka kwa rais aliyemaliza muda wake Yahya Jammeh.Rais huyo wa zamani wa Gambia,awali aligoma kuachilia madaraka.

Rais wa sasa Adama Barrow ameapishwa leo katika nchini jirani kwenye ubalozi wa Gambia ulioko mjini Dakar nchini Senegal na kufuatiwa na shamra shamra ubalozini hapo.
Gambia

 Mpaka sasa haijafahamika wazi lini lini rais mpya wa Gambia ataweza kurejea nchini mwake na kuchukua hatamu za uongozi kwa mara ya kwanza akiwa rais.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments