ADAM BARROW AKABIDHIWA KITI CHA URAIS GAMBIA TAZAMA VIDEO HAPA
Adama Barrow, aliyeibuka mshindi katika uchaguzi wa urais nchini Gambia ameapishwa rasmi kuwa rais wa taifa hilo.
Alikula kiapo hicho katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal huku akiwaagiza wanajeshi wa Gambia kusalia katika kambi zao.
Ametambuliwa kimataifa.
Raia wakifurahia baada ya kupata Rais mpya |
Lakini aliyekuwa rais wa taifa hilo Yahya Jammeh amekataa kujizulu na muda wake wa kuhudumu umeongezwa na bunge.
Viongozi wa Afrika Magharibi wameshindwa kumsihi bw Jammeh kuondoka mamlakani.
Wametishia kumuondoa kwa nguvu.
Bw Jammeh alishindwa katika uchaguzi huo wa Disemba mosi ,kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo.
Lakini anataka matokeo ya uchaguzi huo kufutiliwa mbali akidai makosa mengi katika uchaguzi huo.
''Mimi
Adama Barrow ,naapa kwamba nitatekeleza wajibu wangu katika afisi ya
urais wa taifa la Gambia kwamba nitahifadhi na kutetea katiba'' .
Na
katika hotuba yake ya kuapishwa ,aliwaagiza wanachama wote wa jeshi la
gambia kusalia katika kambi zao. ''Wale watakaopatikana wakibeba silaha
watachukuliwa kuwa waasi'', alionya. TAZAMA VIDEO YA RAIS MPYA WAGAMBIA AKIWA KWENYE KIAPO
Category:
0 comments