JE UNAFAHAMU DONALD TRUMP ATAAPISHWA SAA NGAPI ?TAZAMA RATIBA HAPA
Mshindi wa uchaguzi mkuu wa mwezi
Novemba Donald Trump anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani
Ijumaa tarehe 20 Januari, 2017.
Kisheria, rais anafaa kuapishwa kabla ya saa sita mchana saa za Amerika Mashariki ambazo Afrika Mashariki ni saa mbili usiku.
Hii hapa ni ratiba fupi ya matukio yanayotarajiwa siku hiyo.
Saa 17:30 (Saa za Afrika Mashariki) Wanamuziki walioalikwa wataanza kutumbuiza.19:30 Hotuba za kufungua sherehe zitaanza kutolewa.
20:00 Muda mfupi kabla ya saa Mbili Afrika Mashariki Donald Trump atalishwa kiapo cha kuwa rais wa Marekani na Jaji wa Mahakama ya Juu John Roberts.
Baadaye, kutakuwa na msafara baada ya sherehe ya kuapishwa ambao utaanza katika vidato vya jumba la Capitol Building kuelekea ikulu ya White House kupitia barabara maarufu ya Pennsylvania Avenue.
Bw Trump na mkewe Melania baadaye watacheza densi katika matamasha matatu, mawili katika ukumbi wa mikutano wa Walter E Washington na jingine katika ukumbi wa Jengo la Makumbusho ya Taifa.
Category:
0 comments