BEI YA MAFUTA YA DISEL, MAFUTA YA TAA KUPANDA ,PETROL KUSHUKA KWA SHILLINGI 3 TANZANIA
Akitangaza bei hizo leo Meneja wa Mawasiliano wa Ewura nchini Tanzania , Titus Kaguo aliwaambia wanahabari kuwa petroli imeshuka kwa Sh 3 na itauzwa kwa Sh 2057 kutoka 2060, dizeli imepanda kwa Sh 12, kutoka Sh 1913 hadi 1925 na mafuta ya taa ni Sh 1958 kutoka 1952.
"Mabadiliko haya bei yametokana na bei za mafuta katika soko la dunia kubadilika sanjari na mfumuko wa bei na gharama za usafirishaji ikilinganishwa na mwezi uliopita,"amesema Kaguo.
Hata hivyo mabadiliko hayo ya bei yatatofautiana kutoka mkoa mmoja na mwingine akitoa ufafanuzi meneja wa mawasiliano Ewura alisema mkoa wa Tanga utakuwa na viwango tofauti kidogo na mikoa mingine kutokana na upatikanaji wa mafuta hayo mkoani humo kutokana na uwepo wa bandari inayosaidia urahisi wa meli za mafuta kushusha mafuta hayo mkoani Tanga na kupelekea bei kuwa na unafuu kidogo.
Category:
0 comments