.

.

CLAB YAFUNGIWA TUNISIA KWAKUPIGA MZIKI WENYE ADHANA NDANI YAKE

ZePLAN | 01:58:00 | 0 comments


Imekuwa desturi mbaya kukebei na kuleta dharau katika maswala ya kiimani haswa kwenye mitandao ya kijamii.Klabu moja imejikuta ikiingia matatizoni na kufungiwa kwa kitendo kisichokuwa cha kiuungwana na kukera watu na kusababisha hisia za watu kuja juu kwa kile kinachosadikiwa kuwa Dj husika alipiga nyimbo yenye mchanganyiko na sauti ya adhana ndani ya nyimbo hiyo.
Kupitia kanda ya video hiyo ,video hiyo iliosambazwa siku ya Jumapili kutoka tamasha la Orbit katika eneo la kaskazini mashariki mwa mji wa Nabeul imezua hisia kali katika mitandao ya kijamii.
Klabu
Gavana wa Nabeul, Mnaouar Ouertani alisema kuwa Klabu hiyo itabaki kufungwa hadi pale taarifa zaidi zitakapotolewa kuhusiana na hatma yake.
Uchunguzi umeanzishwa kuhusu kisa hicho.
Image result for orbit club tunisia
Dax J
Kanda hiyo ya video inaonyesha watu waliokwenda kujivinjari katika tamasha hilo siku ya Ijumaa wakicheza densi ya muziki uliokuwa ukichezwa na DJ wawili kutoka bara Ulaya, karibu na hoteli maarufu, Hammamet, ilio ufuoni mwa bahari.
Mziki huo ulijumuisha aina ya densi iliyochanganywa na Adhan, mwito wa Waislamu kwa maombi, mara tano kwa siku.
Image result for orbit club tunisia
" Baada ya kuthibitisha ukweli wa mambo, tuliamua kuifunga klabu hiyo" Bwana Ouertani alikariri
Alisema kuwa meneja wa klabu hiyo amewekwa kizuizini "kwa kukiuka maadili mema yaliozua hisia kali kutoka kwa umma" huku akiongezea kuwa uchunguzi ungali unaendelea.
"Hatutaruhusu mashambulizi dhidi ya hisia za kidini" alisisitiza Bwana Ouertani
Siku ya Jumatatu, waandaji wa tamasha la Orbit waliomba msamaha katika ukurasa wao wa facebook, lakini walisema kuwa hawatokubali kujipa jukumu la kuchezwa kwa muziki wa kupotosha.
DJ "hakujua kwamba ingewakera waliohudhuria kutoka nchi ya Kiislamu kama yetu," walielezea katika ujumbe wao katika mtandao wa kijamii kwa lugha ya kifaransa.
Dax J, aliyecheza Adhan, baadaye aliomba msamaha kwa yeyote yule aliyekerwa na muziki alioucheza katika tamasha la Orbit nchini Tunisia siku ya Ijumaa.
"Haikuwa kupenda kwangu kufadhaisha mtu yeyote," Aliongeza.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments