MORINHO AJITAPA KUHUSU LUKE SHAW BAADA YA KUIBUKA 1-1
Meneja wa timu ya Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa Luke Shaw alitumia mwili wake lakini ubongo wa Mourinho wakati wa mechi kati ya Manchester United na Everton, ambayo ilisha kwa sare ya 1-1.
Shaw mwenye miaka 21, alicheza mara ya kwanza tangu Januari na ilikuwa penalty iliyotokana na mkwaju wake ambapo Zlatan Ibrahimovic alisawazisha.
"Alikuwa mbele yangu na nilikuwa nikimfanyia kila uamuzi" Mourninho alieleza
Shaw ndiye alikuwa mchezaji mdogo pekee kutoka Manchester aliyetengwa kando na Mourinho baada ya United ilitoka bao sare kwa mara ya tisa nyumbani katika ligi msimu huu.
United ilimshukuru Ibrahimovic tena kwa penalty aliyoufunga iliyosaidia United kupata alama moja na kuiweka United nambari tano kwa jedwali.
Category:
0 comments