TRUMP AONYESHA MSIMAMO WAKE JUU YA KOREA KASKAZINI
Marekani imeahidi kuimarisha uwezo wake wa kijeshi ili kukinga washirika wake wa mashariki mwa Asia dhidi ya Korea kaskazini.
Ikulu ya white house inasema rais Trump amemhakikishia waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe kwamba Marekani itasimama pamoja na Korea kusini na Japan, katika kukabiliana na vitisho vya Korea Kaskazini.
Matamshi hayo yanajiri kabla ya mkutano kati ya Rais Trump na rais wa Uchina Xi Jing Ping huko Florida.
Wawili hao wanatarajiwa kujadili kuhusu Korea kaskazini na majaribio ya makombora ya masafa marefu inayoendesha, licha ya umoja wa mataifa kuiwekea vikwazo
Category:
0 comments