.

.

ZANZIBAR YATAFUTA UANACHAMA WA FIFA

ZePLAN | 04:42:00 | 0 comments

Image result for zanzibar national team
Rais wa shirikisho la mpira nchini Tanzania (TFF) Jamal Malinzi, amethibitisha juhudi mpya za Zanzibar kuwa mwanachama wa Fifa.
Zanzibar, ambayo  ni sehemu ya Tanzania inayo jisimamia na kujiendesha yenyewe na  serikali yake, ilipata idhini rasmi na shirikisho la CAF mwezi Machi.
Visiwa vya Zanzibar vimekuwa na matumaini ya muda mrefu kuwa mwanachama wa shiriko la kandanda la kimataifa na maombi yake ya awali yalikataliwa na Fifa mwaka 2005.
Zanzibar national football team Latest news on CECAFA
Shirikisho la kandanda visiwani Zanzibar tayari limetimiza mahitaji muhimu kwa kuwa mashirika ya kitaifa, lazima yawe wanachama wa yale ya bara kabla ya kujiunga na Fifa
Ikiwa Fifa itakubali mwanachama huyo wa 55 wa Caf, basi visiwa vya Zanzibar vitakuwa mwanachama wa 212 wa shirikisho hilo la kandanda duniani.
Atakuwa na haki ya kupiga kura kuamua masuala ya kimataifa ya kandanda na kikosi chake kitakuwa na fursa ya kushiriki mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments