.

.

MITANDAO INAYO ATHIRI ELIMU KWA WANAFUNZI

ZePLAN | 16:31:00 | 0 comments

Tangu kuingia kwa miatandao ya
kijamii nchini vijana wengi wamepata
nafasi ya kuituma au kupokea ujumbe
mfupi, picha na video; kwa njia rahisi
zaidi kuliko ilivyokuwa miaka 20
iliyopita.
Watumiaji wengi wa huduma hiyo
hupendelea zaidi mitandao
inayowawezesha kutuma ujumbe wa siri
kwa njia rahisi, mara nyingi watakavyo
na kwa gharama ndogo. Kati yao, lipo
kundi la wanafunzi linalopendelea
kuwasiliana kwa njia ya kuandikiana
ujumbe wa maandishi na kutumiana
picha.
Kwa mujibu wa takwimu za Machi
mwaka huu za Kampuni ya Utafiti ya
Statista ya Marekani, mtandao wa
Facebook ndiyo unaoongoza kwa kuwa
na watumiaji wengi, ukifuatiwa na
mtandao wa WhatsApp.
Mitandao mingine na idadi ya watumiaji
wake kwenye mabano ni Qzone (watu
milioni 629), Facebook Messenger (watu
milioni 500), WeChat (watu milioni468),
LinkedIn (watu milioni 347), na Twitter
(watu milioni 288).
Pamoja na kuwa Facebook inatawala
orodha ya watumiaji wa mitandao hiyo,
wataalamu wa masuala ya teknolojia ya
mawasiliano wanasema kuwa miaka
michache ijayo vijana wataanza
kukimbilia mitandao mingine yenye
‘ladha’ tofauti.
Baadhi ya mitandao hiyo ni pamoja na
Kik Messenger, ooVoo na WhatsApp
inayowawezesha watumiaji wake
kutuma ujumbe kwa urahisi. Kundi la
vijana wanaopenda kutuma habari
mbalimbali mitandaoni litalazimika
kujikita kwenye mitandao ya Instagram,
Tumblr, Twitter na Vine.
Kundi jingine ni la vijana wanaopenda
kutuma ujumbe wa siri kwa rafiki au
wapenzi wao. Kundi hili linavutiwa
zaidi na mitandao ya Secret-Speak
Freely, Snapchat, Whisper na Yik Yak.
Japokuwa uongozi wa Facebook
umekuwa ukijaribu kuja na mbinu mpya
kila siku ili kuendelea kuwashikilia
wateja wake, bado msukumo wa kizazi
kipya kujaribu mambo mapya unabaki
kuwa uchaguzi pekee.
Kundi la mwisho ni la vijana
wanaotumia muda wao mwingi kwa ajili
ya kuchati na kupeana miadi mtandaoni.
Kundi hili linavutiwa na mitandao ya
MeetMe, Omegle, Skout na Tinder.
Mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika
Chuo Kikuu cha Tumaini, Dar es Salaam
Sunday Elisaria, anasema teknolojia ya
mawasiliano ya simu imeleta matatizo
kwa wanafunzi katika nchi za Afrika
kuliko ilivyotarajiwa.
Elisaria anasema kama mwanafunzi
angetumia simu kama chombo muhimu
cha kumsaidia kupata taarifa za
masomo, wasingelalamikia ukosefu wa
vitabu uliopo katika shule na vyuo
nchini.
“Sasa badala ya mwanafunzi kutumia
mtandao wa ‘google’ kutafuta taarifa za
kitaaluma, muda mwingi anachati na
kutuma picha kwenye ‘Facebook’,”
anasema Elisaria.
Kwa mujibu wa mtandao wa ‘Common
Sense’, wazazi wanatakiwa kuelewa
kuwa mtandao wa ‘Kik Messenger’
unaruhusu vijana kutuma ujumbe bure
bila kikomo kwa haraka.
Watumiaji wa mtandao wa ‘ooVoo’
wanafurahia kuangalia picha za video
bure, huku mtumiaji akiruhusiwa
kuchati na watu hadi 12 bure.
Mtandao wa kijamii ambao pengine ndio
‘habari ya mjini’ hivi sasa wa
‘WhatsApp’, unamwezesha mtumiaji
kutuma ujumbe, sauti, video na picha
kwa mtu mmoja au wengi. Moja ya
masharti ya ‘WhatsApp’ ni kuwa
mtumiaji lazima awe na umri wa miaka
zaidi ya 16.
Mwanafunzi wa Shule ya Sheria ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, Edna John
anasema wanafunzi wanaotumia
‘Facebook’ wameanza kuvutiwa na
mtandao wa kijamii wa ‘Instagram’ kwa
kuwa unamwezesha mtumiaji kupiga
picha, kuzihariri na kuziweka
mtandaoni. Pia unamwezesha mtumiaji
kuweka video yenye sekunde 15.
‘Twitter’ inamwezesha mtumiaji kutuma
ujumbe mfupi wa herufi 140. Mara
nyingi hutumiwa na watu wazima
ambao hupendelea kutuma ujumbe wa
wazi, ingawa inawezekana pia kutuma
ujumbe wa siri.
Mitandao hatari kwa vijana
Mitandao ya ‘Secret-Speak Freely’,
‘Snapchat’, ‘Whisper’ na ‘Yik Yak’,
inatajwa kuwa ni hatari kwa vijana kwa
sababu inawaruhusu kutumiana ujumbe
wa siri au kutamka maneno yoyote
wanayoyataka wakiwa na uhakika kuwa
hakuna atakayewagundua.

Toa maoni yako:
Ochec54@gmail.com

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments