.

.

KENYA WASHAMBULIA SOMALIA

ZePLAN | 02:34:00 | 0 comments

Ndege za kijeshi za Kenya zimeshambulia
maeneo ya wapiganaji wa kundi la Alshabaab
katika taifa jirani la Somalia ,msemaji wa jeshi
ameiambia BBC.
Ndege hizo zililenga maeneo mawili ya jimbo la
Gedo,linalotumiwa na wapiganaji hao kuvuka na
kuingia Kenya, msemaji huyo ameongeza.
Maeneo hayo mawili hutumiwa na wapiganaji hao
kupanga mshambulizi nchini Kenya.
Wanajeshi wa AMISOM walitarajiwa kupeleka
wanajeshi wao katika eneo hilo la Gedo lakini
hadi sasa hawajafanya hivyo.
Hili ni shambulio la kwanza la Kenya kwa
shambulizi la alshabaab ambalo lilisababisha
mauaji ya watu 148 katika chuo kikuu cha
Garissa wiki iliopita.
Amisom
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameapa kujibu
shambulizi hilo kwa njia mbaya zaidi.
Msemaji wa jeshi la Kenya David Obonyo
ameiambia BBC kwamba Jeshi la Kenya lilijibu
vitisho kwa kutekeleza mashambulizi ya angani
siku ya jumapili usiku katika eneo hilo.
Hakuna maelezo zaidi ya oparesheni hiyo
yaliotolewa.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments