.

.

MAMBO YAWA MAZITO DODOMA

ZePLAN | 04:16:00 | 0 comments


Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Mrisho Kikwete 
   
Dodoma. Mambo yanaonekana kuwa mazito kwa CCM ambayo inajiandaa kufanya moja ya mikutano yake muhimu ya Vyombo hivyo vya juu vya CCM, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu vitakutana kuanzia kesho kupanga utaratibu wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu, huku vikitakiwa kufanya maamuzi mazito kuhusu makada wanaotaka kuwania urais ambao wamefungiwa pamoja na mawakala ambao wamekuwa wakiendesha kampeni za kutaka wagombea hao waungwe mkono.
 
Vikao hivyo vinafanya kazi ya kuandaa na kuthibitisha ajenda za vikao vikuu huku ajenda muhimu katika mikutano hiyo ikiwa ni hali ya kisiasa nchini, maandalizi ya uchaguzi mkuu, mchakato wa namna ya kuwapata wagombea wa CCM wa ngazi zote na ratiba ya uchaguzi.
Vikao hivyo pia vitapewa taarifa ya maandalizi ya ilani ya chama na kutoa maoni.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments