.

.

Morogoro:watu kumi washikiliwa kwa tuhuma za ugaidi

ZePLAN | 00:42:00 | 0 comments

Watu 10 wanashikiliwa na polisi mkoani
Morogoro baada ya kukamatwa msikitini wakiwa
na milipuko 30, sare za jeshi na bendera nyeusi
inayodaiwa kutumiwa na kundi la wapiganaji wa
Al Shabaab wa nchini Somalia.
Katika tukio hilo, mmoja anayesadikiwa kuhusiana
na watu hao waliokamatwa aliuawa na wananchi
wenye hasira baada ya kumjeruhi kwa panga
askari polisi aliyekuwa akipambana naye.
Akizungumza na waandishi wa habari leo,
Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Leonald
Paul alisema tukio hilo limetokea jana (Aprili 14)
majira ya saa 3.30 usiku katika kitongoji cha
Nyandero, tarafa ya Kidatu wilayani
Kilombero.Kamanda Paul alimtaja mtu aliyefariki
kuwa ni Hamad Makwendo ambaye umri wake
haujafahamika ambaye ni mkazi Manyasini Ruaha
wilayani Kilombero.
Aidha alisema siku ya tukio polisi walipata taarifa
kutoka kwa raia wema kuhusu watu hao na
kwamba walitaarifiwa kuwa wanajihusisha na
matukio mbalimbali ya uhalifu na polisi waliamua
kufatilia nyendo zao.
Kamanda akionesha vilipuzi
Akisimulia tukio hilo, Kamanda Paul alisema:
“Polisi walipata taarifa kuwa watu hao walitumia
usafiri wa bajaji mbili kwenda kusikojulikana na
wakati wakiendelea na zoezi la kufuatilia ndipo
walikutana na bajaji moja ikiwa na abiria mmoja
ambaye ni Mkwendo na kuisimamisha.”
Alisema kuwa bajaji hiyo iliposimama marehemu
huyo aliruka na kuanza kukimbia ndipo askari
mwenye namba F .3323 Koplo Nasoro alianza
kumkimbiza na alipomkaribia mtuhumiwa huyo
alichomoa jambia alilokuwa nalo na kumkata
askari huyo eneo la shingoni.
Askari mwingine mwenye namba E.9245 Koplo
Chomola ambaye alikuwa nyuma alifanikiwa
kumpiga risasi ya mguu mtuhumiwa huyo,
ambapo alipoanguka chini wananchi wa eneo hilo
tayari walifika katika eneo hilo na kuanza
kumshambulia marehemu huyo kisha kumchoma
moto kwa hasira.
Kamanda huyo alisema walianza kuwasaka watu
wengine ambao walipata taarifa wapo katika
Msikiti wa Suni uliopo Kidatu.
“Polisi walipofika katika msikiti huo waliuomba
uongozi wa msikiti huo kuwatoa watu wote
waliokuwa msikitini ili kuweza kubaini watu
ambao wanatiliwa mashaka.”
Alisema polisi walendelea na ukaguzi na
kuwakamata watu hao 10 wakiwa na vifaa hivyo
na kuwatia nguvuni.
Baadhi ya vifaa vilivyokamatwa msikitini na
polisi ambapo watu 10 wanashikiliwa na jeshi
hilo mjini Morogoro.
Kamanda huyo alitaja vitu vilivyokutwa katika
mabegi yaliyokuwa ndani ya msikiti huo ni
pamoja na milipuko 30, bendera nyeusi yenye
maandishi ya Kiarabu yakisomeka ‘Mungu
Mmoja’, majambia, bisibisi, vinyago vya kuziba
uso (masks), nguo za jeshi, misumeno ya chuma
na spana.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments