IRAQ:kiongozi wa kundi la IS auwawa
Runinga nchini Iraq imeripoti kuwa Izzat Ibrahim
al-Douri, ambaye wakati mmoja alikuwa
makamu wa Rais Saddam Hussein na mmoja
wawaanzilishi wa kundi la Islamic State nchini
Iraq, ameuawa.bado hakuna taarifa rasmi ya kuthibitisha
kifo chake, lakini picha na maelezo kuhusu kifo
cha Bwana Al Douri imeripotiwa pakubwa.
Iwapo taarifa hiyo ni kweli, kifo chake kitakuwa
hatua kubwa kwa serikali ya Iraq dhidi ya
makundi ya Jihadi.
Al Douri ambaye daima ana masharubu mekundu,
alikuwa mfalme katika kilabu kwenye kadi
zilizotolewa ili kusaidia majeshi ya Marekani
kutawambua wanachama katika utawala wa
Saddam Hussein, mnamo mwaka 2003
Category:
0 comments