Somalia kushiriki katika kombe la Africa 2019
Rais wa shirikisho la soka nchini Somalia Adbi
Qani anatumai kwamba taifa lake litashiriki
katika michuano ya kombe la Afrika mwaka
2019 na kumaliza kiu ya taifa hilo tangu mwaka
1974.
Walishiriki katika kombe la mataifa ya Afrika mara
moja kutokana na ghasia za kisiasa,ukosefu wa
fedha na miundo msingi mibovu.
Pamoja na Eritrea nchi hizo mbili hazitashiriki
katika mechi za kufuzu za mwaka 2017.
Ni mataifa hayo mawili katika shirikisho la soka
barani afrika CAF yatakayokosa kushiriki.
Lakini Qani anaamini kwamba huu uwanja mpya
ukitarajiwa kumalizwa kujengwa baadaye mwaka
huu ,taifa hilo hilo linajiandaa kurudi katika
michuano hiyo kabla ya kukamilika kwa muongo
huu.
Category:
0 comments