.

.

USAFIRI WA TRENI ,DAR MPAKA KIGOMA WAZINDULIWA UNAONI GANI

ZePLAN | 07:03:00 | 0 comments

Dar es Salaam. Treni ya kisasa (Delux),
kwenda Bara yenye mabehewa 22
ilianza safari yake ya saa 30 kutoka Dar
es Salaam kwenda Kigoma ikiwa ni
tofauti ya saa sita ikilinganishwa na
safari ya treni ya zamani.
Kutokana na tofauti hiyo, abiria
walioanza safari kwa furaha na
matumaini jana saa tano asubuhi
wanatarajiwa kufika Kigoma leo saa 11
jioni badala ya saa tano usiku.
Hata hivyo, abiria hao watalazimika
kuingiza mikono yao zaidi mifukoni,
kutokana na kiwango kipya cha nauli
kuwa Sh79,400 badala ya Sh75,700 za
awali kwa daraja la kwanza.
Huku nauli za daraja la pili ikishuka
kutoka Sh55,400 hadi Sh,47,600 zile za
daraja la tatu zimepanda kutoka
Sh27,700 hadi Sh35,700.
Kwa mtazamo wa haraka, mabehewa
hayo yanavutia yakilinganishwa na yale
ya awali yaliyokuwa yamekithiri kwa
uchakavu, yaliyokuwa yamejaa mende
na yenye milango na madirisha mabovu.
Mabehewa hayo yana viti vya kutosha,
huduma ya intaneti, swichi za umeme za
kuchajia simu na kuunganisha
kompyuta na safari zake zimeongezeka
kutoka mbili hadi tatu kwa wiki.

Akizungumza muda mfupi kabla
uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Reli Tanzania (TRL), Mhandisi
Kipallo Kisamfu alisema wamelazimika
kupandisha viwango vya nauli kutokana
na gharama zitakazokuwa zinatumika
katika uendeshaji wa treni hiyo.
“Licha ya kuongeza kidogo kiwango cha
nauli, dhamira yetu ni kuwapatia abiria
huduma safi na ya raha... kila msafiri
atasafiri akiwa ameketi kwenye kiti
chake. Hakuna abiria atakayesafiri
akiwa amesimama,” alisema na
kuongeza: “Treni inayozinduliwa leo
inatumia mabehewa mapya 22
yaliyonunuliwa kutoka Korea Kusini na
kichwa cha treni kiliundwa upya kwenye
karakana ya TRL iliyopo Morogoro
mabehewa mapya yamegharimu Serikali
Sh28.6 bilioni.”
Kuhusu vituo vya ambavyo treni hiyo
alisema itasimama kwenye vituo
vikubwa ambavyo vingi ni vile vya miji,
wilaya na mikoa.
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dk
Shabaan Mwinjaka aliwataka abiria
kuwa walinzi wa treni hiyo ili
kuhakikisha usafiri huo unadumu.
“Kumekuwa na tabia ya watu kujiamulia
kuharibu mali za umma, ninawaomba
abiria mtakaopanda treni hii muwe
walinzi wa wenzenu kwa sababu baadhi
ya abiria wamekuwa na tabia ya
kuchora kwenye viti,” alisema Dk
Mwinjaka.
Mmoja wa abiria, Saida Roman alisema
Serikali inahitaji kupewa pongezi kwa
hatua hiyo kwani hivi sasa abiria
wanaotumia usafiri wa treni kutoka Dar
es Salaam kwenda Kigoma watasafiri
kwa raha tofauti na ilivyokuwa zamani.

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments