.

.

AL SHABAAB YATEKA MSIKITI GARISSA

ZePLAN | 04:36:00 | 0 comments

Al Shaabab waliuteka msikiti mmoja katika kaunti ya Garissa kwa muda na kuonya wenyeji dhidi ya kuisaidia serikali ya Kenya na ujasusi
Viongozi Kaskazini mwa Kenya wamesema kuwa wapiganaji wa kundi la kigaidi kutoka Somalia la Al Shaabab waliuteka msikiti mmoja katika kaunti ya Garissa kwa masaa kadhaa.
Wapiganaji hao waliwahutubia waumini waliokuwa msikitini kwa karibu saa mbili kabla ya kutokomea mwituni.
Waliikosoa serikali ya Kenya na kuonya waumini dhidi ya kuwa majasusi wa serikali ya Kenya.
Mwezi uliopita Al Shaabab walivamia chuo kikuu cha Garissa na kuwaua watu 150 wengi wao wanafunzi.
Majeshi ya Kenya ni miongoni mwa kikosi cha kulinda amani cha muungano wa Afrika Amisom
Kundi hilo kutoka Somalia linaaminika kuwa na wafuasi nchini Kenya ambapo limetekeleza mashambulizi kadha katika jitihada ya kuilazimisha serikali ya Kenya kuondoa majeshi yake nchini Somalia.
Majeshi ya Kenya ni miongoni mwa kikosi cha kulinda amani cha muungano wa Afrika Amisom ambao wanaisaidia serikali dhaifu ya Somalia kupigana na waasi wa Al Shabaab

Category:

About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!

0 comments