KADI ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA NI MARUFUKU TANZANIA
Serikali ya Tanzania imepiga marufuku utengenezaji wa kadi za Krismasi na Mwaka Mpya kwa gharama ya serikali au pesa za umma.
Taarifa
kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue imesema afisa yeyote wa
serikali anayepanga kuchapisha au kutengeneza kadi kama hizo anafaa
kufanya hivyo "kwa gharama zake mwenyewe”.Hatua hiyo inaonekana kuwa ya karibuni zaidi kwa serikali kubana matumizi tangu kuingia madarakani kwa Rais John Pombe Magufuli mapema mwezi huu.
"Fedha zilizopangwa kugharamia utengenezaji na uchapishaji wa kadi, zitumike kupunguza madeni ambayo Wizara, Idara na Taasisi za umma zinadaiwa na wananch/wazabuni waliotoa huduma na bidhaa kwao au zipelekwe katika matumizi mengine ya kipaumbele,” imesema taarifa iliyotoka kwa kaimu mkurugenzi wa mawasiliano ya Ikulu Bw Gerson Msigwa.
Category:

0 comments